Mjasiriamali anajengwaje?

Vitu vinavyomjenga mjasiriamali ni pamoja na vifuatavyo:

FULSA
Fulsa ni kama uti wa mgongo kwa mjasiliamali. mjasiliamali lazima awe na uwezo wa kutambua au kugundua fulsa, uwezo wa kuchambua na kuchanganua fulsa pia kuchukua hatua juu ya fulsa husika.

MTAJI
ni kitu chochote ambacho mjasiliamali anawezatumia katika kuzalishia au kufanyia jambo flani kwa lengo la kupata faida. mtaji umegawanyika katika miundo ifuatayo:- mtaji wa fedha,nguvu kazi,mtaji jamii,elimu na utaalamu katika jambo flani.


UBUNIFU
Kwa kawaida mjasiliamali anatakiwa kuwa mbunifu, ubunifu ndio unamtofautisha mtu mmoja na mwingine hata kama wote watafanya jambo linalo fanana. kilasiku unatakiwa kufikili ni jinsi gani utafanya jambo jipya ua jambo lililofanya na wengine lakini wewe ufanye katika njia tofauti.

MAWASILIANO
Mawasiliano huunganisha vitu pamoja ana huweka watu pamoja na husaidia kupata taarifu huhimu  katika biashara yako.Mawasiliana huunganisha mtaji, fulsa na ubunifu, mjasiliamali anatakiwa kuboresha mawasiliano ili afanikiwe katika ujasiliamali wake.